• Skip to secondary menu
  • Skip to content
  • Skip to footer

Clouds Check

Tenganisha Ukweli na Tetesi | Habari Clouds

  • Entertainment
  • Local News
  • Business News
    • Money & Finance
  • Sports
  • Science
  • Tech News
  • Travel
  • Health & Fitness
  • World
  • Environment

JE VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO VINAPUNGUA TANZANIA?

May 17, 2018 by khadijamahanga Leave a Comment

umatano Februari 28, 2018 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alizindua ripoti ya makadirio ya watu nchini Tanzania inaonyesha ongezeko la watu kufikia watu milioni 54.2 huku ikikadiriwa idadi ya watu nchini Tanzania itafika takribani Milioni 77.5 ifikapo mwaka 2030

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ongezeko hilo linatokana (pamoja na sababu nyinginezo) uwepo wa idadi kubwa ya vizazi inayofikia milioni 2 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo inayotajwa kufikia 400,000 kwa mwaka lakini pia kupungua kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano

#CloudsCheck imefuatilia kwa kina suala la vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini ili kutaka kubaini kama kuna ongezeko au punguzo na mchango wake katika kuongezeka kwa idadi ya watu nchini.

Ripoti kadhaa za mashirika ya kimataifa zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano nchini.

Ripoti ya benki ya dunia (World Bank) inaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 nchini Tanzania. Ripoti hiyo inaonyesha kupungua kwa idadi ya vifo kutoka 179 kati ya kila watoto 1,000 mwaka 1990, kufikia 132 mwaka 2000, 72 mwaka 2010 hadi watoto 57 mwaka 2016

(Takwimu kwa mujibu wa benki ya Dunia)

Ripoti ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaonyesha pia kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania. Ripoti hiyo inaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya vifo kutoka 166 kati ya watoto 1,000 mwaka 1990 hadi kufikia 112 mwaka 2005 na 67 mwaka 2015

(Takwimu kwa mujibu wa UNICEF)

Kutokana na ripoti hizi, #CloudsCheck inahitimisha kuwa ni wazi kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano ni moja kati ya mambo yanayochangia kuongezeka kwa idadi ya watu nchini kama ilivyoelezwa katika ripoti ya makadirio ya watu nchini Tanzania. Hivyo NI KWELI kupungua kwa vifo kwa watoto chini ya miaka mitano nchini kunachangia kuongezeka kwa idadi ya watu nchini

Filed Under: Uncategorized

Reader Interactions

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Footer

Je, unahitaji tuhakikishe usahihi na ukweli wa habari au taarifa yoyote: Tutumie kwa barua pepe:

info@cloudsmedia.co.tz

Au kwa namba: +255 (0)22 278 1445

Other Projects:

  • HURUmap Tanzania
  • Open Data TZ

Join our community:

  • HacksHackers Africa

Copyright © 2019 · Lifestyle Pro on Genesis Framework · WordPress · Log in